Rais William Ruto amefafanua kuwa ardhi ambapo kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote kinajengwa inamilikiwa kisheria na serikali. Hii inafuatia madai kutoka kwa baadhi ya watu wanaotaka fidia kwa misingi ya umiliki wa ardhi hiyo. Ruto alisema kuwa iwapo sehemu yoyote ya kiwanda hicho itapanuka na kuingia katika ardhi binafsi inayomilikiwa kisheria, serikali ndiyo itakayohusika na kuwalipa fidia wamiliki walioathirika, na si mwekezaji.

WILLIAM RUTO-LAND