Chama cha ODM hii leo kitaendesha hafla ya kitaifa ya kuwasha mishumaa kuadhimisha mwaka mmoja tangu kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga. Hafla hiyo itafanyika saa kumi na mbili jioni, huku Wakenya humu nchini na ng'ambo wakialikwa kuwasha mishumaa katika makao makuu ya kaunti na maeneo mengine yaliyotengwa. ODM ilisema kuwa hafla hiyo inaandaliwa kwa ushirikiano na Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi inayoratibu maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kifo cha Raila. Hafla hiyo itaashiria kuzinduliwa kwa mpango wa mwezi mzima wa kusherehekea urithi wake.