Mwanamume mwenye umri wa miaka 31 kutoka Kisumu amehukumiwa kifungo cha miaka 35 gerezani kwa kumuua shangazi yake kufuatia mzozo wa kifamilia. Kulingana na taarifa kutoka kwa DPP, mwanamume huyo alihukumiwa na Mahakama Kuu ya Kisumu baada ya Jaji Joe Omido kumpata na hatia kwa kosa la kumuua shangazi yake mwaka 2023, katika eneo dogo la Kapuonja, Kaunti Ndogo ya Kisumu Magharibi. Alishtakiwa kwa kosa la mauaji.