Gavana wa Mombasa Abdul Nassir ameitetea serikali pana dhidi ya madai ya upinzani kwamba inakiuka Katiba. Akizungumza wakati wa utoaji wa hati miliki na Rais William Ruto huko Mombasa, Nassir alisema utawala umepatia kipaumbele ujumuishaji, huduma ya afya na utatuzi wa dhuluma za kihistoria za ardhi. Alibaini kuwa haya pia yalikuwa miongoni mwa masuala muhimu yaliyopigiwa upatu na Waziri Mkuu wa zamani marehemu Raila Odinga, huku nchi ikijiandaa kuadhimisha kumbukumbu ya kwanza ya kifo chake.
ABDUL SWAMAD-DEFEND