Serikali inaongeza juhudi za kuimarisha uzalishaji wa mafuta nchini na kupunguza utegemezi wa mafuta yanayoingizwa kutoka nje. Katibu wa Idara ya Petroli Mohammed Birik, alisema serikali itaendelea kushirikiana na taasisi muhimu ili kuimarisha sera na kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya shughuli za utafutaji, uzalishaji na uuzaji wa mafuta. Pia alitangaza kuwa shughuli za utafutaji wa mafuta katika eneo la South Lokichar zinatarajiwa kuanza mwezi Disemba.

MOHAMMED BIRIK-OIL