Takriban asilimia 63 ya ardhi ya kilimo nchini Kenya ina tindikali, huku karibu ekari milioni saba zikiwa na kiwango kikubwa cha tindikali, amesema Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe. Ili kukabiliana na hali hiyo, serikali inaanzisha mfumo wa kitaifa wa kupima na kuchora ramani ya udongo ili ushauri kuhusu matumizi ya mbolea na misaada kwa wakulima viendane na hali ya ardhi ya kila mkulima. Kagwe alisema nchi haiwezi tena kutumia mapendekezo ya aina moja ya mbolea kwa udongo unaotofautiana katika viwango vya virutubisho na tindikali.
MUTAHI KAGWE - TUMIA