Tume ya Kitaifa ya Ardhi imewahakikishia wakaazi wa Pwani kwamba itafuatilia dhulma za kihistoria za ardhi hadi mwisho, huku ikionya kwamba baadhi ya kesi zinaweza kuchukua zaidi ya miaka 10 kutatuliwa. Mwenyekiti wa NLC Abdullahi Alawy alisema tume hiyo imejipanga kushughulikia malalamiko ambayo yamewalemea wakaazi wa Pwani. Alawy aliwasihi watu walio na kesi zinazosubiriwa kutopoteza matumaini na kuwashauri kuhakikisha wana hati sahihi za umiliki.