Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang'ula anasema Bunge litaweka kipaumbele mageuzi ya uchaguzi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2027. Wetang'ula alisema amepeleka mapendekezo yaliyowasilishwa na IEBC kwa Kamati ya Haki na Masuala ya Kisheria kwa ajili ya kuzingatiwa. Kamati hiyo inatarajiwa kupendekeza marekebisho ya kuingizwa katika Mswada wa Marekebisho ya Uchaguzi Nambari Mbili, ambao ni miongoni mwa mambo ya kipaumbele kwa kikao cha sasa. Aliwasihi wabunge kuharakisha mchakato huo.
MOSES WETANGULA - PRIORITY