Watu wenye umri wa miaka 40 na zaidi, au wale walio na historia ya familia ya shinikizo la damu au kisukari, wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa kila mwaka wa viwango vya sukari na kolesteroli kwenye damu. Daktari wa magonjwa ya moyo Duncan Kilingo anasema uchunguzi ni muhimu kwa kugundua mapema, akibaini kuwa takriban asilimia 70 ya watu wenye shinikizo la damu hawajui wana ugonjwa huo. Anasema dalili za ugonjwa wa moyo na mishipa ni pamoja na maumivu ya kifua, upungufu wa pumzi na uchovu usio wa kawaida. Ushauri huo unakuja wakati dunia inaadhimisha Siku ya Moyo Duniani.

DUNCAN KILINGO – TREATMENT