Polisi katika Kaunti ya Kilifi wamemkamata mwanamke mwenye umri wa miaka 31 baada ya kupatikana akifanya mfungo wa muda mrefu huko Shakahola, Malindi, Kaunti ya Kilifi. Eneo hilo limekuwa likifuatiliwa kwa karibu baada ya miili zaidi ya 400 kufukuliwa kutoka makaburi ya kina kifupi kufuatia vifo vilivyohusishwa na dhehebu la kidini. Mwanamke huyo, ambaye ni mkaazi wa Thika, anaripotiwa kuonekana na wakaazi wa eneo hilo akifunga kwa siku tatu karibu na Mto Galana, maafisa walisema.