Mbunge wa Embakasi Mashariki, Babu Owino, anasema rekodi yake Bungeni inampa sifa za kuwania kiti cha Gavana wa Nairobi katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Babu, ambaye anatarajia kumrithi Gavana Johnson Sakaja, alisema utendakazi wake kama mbunge unaonyesha uwezo wake wa kutoa suluhisho la vitendo kwa changamoto zinazowakabili wakaazi. Alisema wakaazi wa Nairobi wanajali zaidi utoaji wa huduma na kwamba rekodi yake inaonyesha anaweza kutimiza hilo iwapo atachaguliwa kuwa gavana.

BABU OWINO - RANKED