Washirika wa Rais William Ruto katika Kaunti ya Makueni wanamsihi kiongozi wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka, kuzingatia kushirikiana na serikali ya Kenya Kwanza kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Viongozi hao, wakiongozwa na Mbunge wa Kibwezi Magharibi Mwengi Mutuse, walikaribisha kauli ya Kalonzo kuhusu uwezekano wa kushirikiana na Ruto, lakini wakamtaka aanze mazungumzo na Rais kabla ya uchaguzi badala ya kusubiri hadi baada ya uchaguzi huo.

MWENGI MUTUSE – KALONZO