Kesi ya mauaji inayomkabili Sarah Wairimu, ambaye anashutumiwa kwa kumuua mumewe marehemu Tob Cohen, inaendelea tena leo asubuhi, huku upande wa mashtaka ukitarajiwa kuita mashahidi zaidi. Shilindwa Shihemi, aliyekuwa mfanyakazi wa bustani na wa ndani katika makaazi ya wawili hao huko Lower Kabete, jana alisimulia tukio hilo la mwezi Februari 2019 ambapo Cohen alikuwa akivuja damu na kumwomba apige picha majeraha yake.

SHILINDWA SHIHEMI – TESTIMONY