Rais William Ruto ametangaza kuwa upanuzi wa mradi wa maji wa Chemchemi za Mzima katika Kaunti ya Taita-Taveta utaanza mwaka huu. Rais alisema Serikali itatafuta na kutoa shilingi bilioni 30 kwa ajili ya mradi huo ili kukabiliana na tatizo sugu la uhaba wa maji katika kaunti hiyo na maeneo jirani. Mradi huo, utakaofadhiliwa kupitia Hazina ya Kitaifa ya Miundombinu, utasambaza maji katika maeneo bunge ya Mwatate, Voi na Taveta, na pia kupeleka maji jijini Mombasa.
WILLIAM RUTO – TAITATAVETA