Polisi wanachunguza tukio ambapo wanaume watatu huko Kirinyaga waliripoti kuleweshwa na kitu kisichojulikana kabla ya kupoteza vitu vya thamani na pesa katika hoteli moja mjini Sagana. Tukio hilo liliripotiwa katika Kituo cha Polisi cha Sagana Jumamosi. Kulingana na polisi, wanaume hao walikutana na wanawake watatu wasiowajua katika eneo hilo la burudani. Wanaume hao watatu walisema waliamka yapata saa sita mchana Jumamosi na kujikuta peke yao, na kugundua kuwa walikuwa wameibiwa mali zao kama vile simu na vipatakilishi.