Kiongozi wa Chama cha Jubilee, Fred Matiang’i, anatoa wito wa umoja miongoni mwa viongozi wa upinzani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Mating'i anasema upinzani lazima uendelee kuwa na umoja bila kujali ni nani atakayechaguliwa hatimaye kuwa mgombea urais wa upande huo. Anasema msisitizo unapaswa kuwa katika kushirikiana, bila kujali matamanio ya watu binafsi, huku vyama vya upinzani vikijiandaa kwa uchaguzi ujao.
FRED MATIANG’I – OPPOSITION