Waziri wa Usalama, Kipchumba Murkomen, anasema serikali inaongeza idadi ya maafisa wa usalama na vifaa katika maeneo ya mipaka kati ya Turkana na West Pokot pamoja na Turkana na Baringo, katika juhudi za kurejesha amani ya kudumu. Murkomen anasema operesheni hizo zitalenga wahalifu na washirika wao, silaha haramu na mifugo iliyoibiwa, huku zikishughulikia migogoro inayotokana na ushindani wa rasilimali.
KIPCHUMBA MURKOMEN – SECURITY