IEBC imekanusha ripoti kwamba inawasajili raia wa kigeni kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027, ikielezea madai hayo kuwa ya kupotosha na yasiyo na msingi. Tume hiyo inasema hakuna ushahidi wa kuaminika uliowasilishwa kuthibitisha madai ya usajili haramu wa wapiga kura au uhamisho wa wapiga kura. IEBC imefafanua kuwa jukumu lake ni kuwasajili raia wa Kenya wanaostahiki na walio na nyaraka halali za utambulisho pamoja na kutunza daftari la wapiga kura.