Katibu wa Usalama, Raymond Omollo, ametetea msimamo wa serikali kuhusu maendeleo ya taifa, akisisitiza kuwa rasilimali na huduma za umma lazima ziwafikie Wakenya bila ubaguzi wowote wa kikanda, kijamii au kisiasa. Akizungumza katika hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya maendeleo ya kanisa eneo la Narok Mashariki, Omollo alisema Rais William Ruto ameweka kiwango kipya cha uongozi kupitia kile alichokitaja kuwa ni mkakati wa maendeleo ya taifa usio na ubaguzi na unaojumuisha watu wote.
RAYMOND OMOLLO - ZUNGUMZIA