Kaunti ya Kisii imeimarisha juhudi za kudumisha usafi katika miji yake kwa kuzindua mapipa ya taka yenye rangi tofauti, hatua inayorahisisha na kuboresha ufanisi wa kutenga taka. Gavana Simba Arati alisema kuwa sehemu kubwa ya taka katika kaunti hiyo ni za asili organic na zinaweza kutumika kwa tija iwapo zitatenganishwa ipasavyo katika hatua ya awali. Aliongeza kuwa kaunti hiyo inaachana na utaratibu wa kutumia maeneo ya kutupia taka na badala yake inaelekea kwenye mfumo wa uchumi wa mzunguko, ambapo taka hutumika tena, huwa recycled na kurejeshwa katika matumizi.
SIMBA ARATI - IMPLEMENT