Naibu Inspekta Jenerali wa polisi Gilbert Masengeli amelaani uharibifu wa mali wakati wa matukio ya kisiasa, akihoji ni kwa nini Wakenya huchoma magari ya raia wenzao. Masengeli alitoa mfano wa kijana ambaye gari lake jipya alilonunua kwa mkopo, liliharibiwa Embu wiki iliyopita. Aliwasihi Wakenya kuheshimu haki na mali za watu wengine, akionya kwamba vurugu za kisiasa zinatishia amani na mshikamano wa kijamii kabla ya uchaguzi wa 2027.
GILBERT MASENGELI - VIOLENCE