Mamlaka ya IPOA imeanzisha uchunguzi kuhusu kuvurugika kwa mkutano wa wajumbe wa UDA katika Uwanaj wa Nembure huko Embu siku ya Jumamosi. Kamishna wa IPOA John Muchiri alisema uchunguzi huo unafuatia ripoti za matumizi ya nguvu kupita kiasi na polisi walipokuwa wakikabiliana na vijana na kusababisha machafuko. Tukio hilo, wakati wa mkutano ulioongozwa na Naibu Rais Kithure Kindiki, lilisababisha mtu mmoja kufariki, maafisa kadhaa wa polisi wakajeruhiwa na magari kuchomwa moto.

JOHN MUCHIRI - FAMILIES