Tume ya IEBC imewaonya wanasiasa dhidi ya matamshi ya kiholela ambayo yanaweza kudhoofisha mamlaka na uaminifu wa tume ya uchaguzi. Kamishna Alutalala Mukhwana alipinga matamshi ya hivi karibuni yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa UDA Hassan Omar ambaye alidai kwamba hata wafu wangempigia kura Rais William Ruto kushinda. Alitoa onyo hilo wakati wa Mkutano wa Amani ulioandaliwa na NCIC.

ALUTALALA MUKHWANA - TAHADHARI