Ziara ya maendeleo ya siku tano ya Rais William Ruto katika eneo la Luo Nyanza inaingia siku yake ya pili leo, ambapo anatarajiwa kukagua miradi kadhaa yenye thamani ya mabilioni ya pesa iliyoanzishwa na serikali yake, huku pia akilenga kuimarisha uungwaji mkono wake wa kisiasa katika ngome ya chama cha ODM kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027. Kwa mujibu wa ratiba yake, leo Rais Ruto atafanya mkutano wa faragha na takriban watu elfu 10 kutoka kaunti za Kisumu, Siaya, Homa Bay na Migori; mkutano ambao pia utahudhuriwa na viongozi waliochaguliwa kutoka eneo hilo.