Wataalamu wa afya wametoa wito wa kuchukua hatua za kina katika kuzuia na kudhibiti kisukari cha type 2, unene kupita kiasi na matatizo mengine yanayohusiana nayo. Wakizungumza wakati wa utambulisho wa dawa za Ozempic (kwa ajili ya kisukari cha aina ya 2) na Wegovy (kwa ajili ya kudhibiti uzito), wataalamu hao walisisitiza umuhimu wa utambuzi wa mapema, matibabu sahihi na uangalizi wa muda mrefu. Hafla hiyo pia ilisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika kuimarisha mifumo ya afya na kuboresha upatikanaji wa matibabu kwa watu wanaoishi na kisukari pamoja na tatizo la unene uliopitiliza.

VOX POP-APPROACH