Wataalamu wa afya wameelezea wasiwasi wao kuhusu ongezeko la mzigo wa ugonjwa wa kisukari nchini Kenya, wakionya kuwa watu wengi wanaishi na ugonjwa huo bila kufahamu. Daktari wa mfumo wa homoni (endocrinologist), Roseline Ngugi, anasema kuwa uchunguzi na utambuzi wa mapema ni muhimu katika kuzuia madhara makubwa na kuboresha matokeo ya matibabu. Alibaini kuwa kiwango cha maambukizi ya kisukari barani Afrika kimeongezeka kwa zaidi ya asilimia 142 katika muongo uliopita, huku zaidi ya asilimia 60 ya visa nchini Kenya vikiwa havijagunduliwa.
ROSELINE NGUGI-DIABETES