Washirika wa kisiasa wa Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua wameongeza ukosoaji dhidi ya utawala wa Rais William Ruto kufuatia matukio ya vurugu yaliyoripotiwa Embu Jumamosi. Akizungumza katika Kanisa la ACK Witima, Katibu Mkuu wa DCP John Methu alihoji jinsi serikali ilivyoshughulikia vurugu hizo na madai ya kuhusika kwa polisi. Viongozi hao pia walimtetea Mbunge wa Manyatta Gitonga Mukunji, ambaye amehusishwa na machafuko hayo na kuhoji ni kwa nini Kindiki alishindwa kuzuia usumbufu huo licha ya madai ya kuwepo ujasusi kuhusu shambulio lililopangwa.

JOHN METHU-QUESTION