Wakaazi wa eneo la Budalangi, ambalo hukumbwa mara kwa mara na mafuriko, wanatoa wito wa kuwepo kwa uelewa zaidi kuhusu afya ya akili na msaada wa kisaikolojia na kijamii huku nchi ikijiandaa kwa mvua inayotarajiwa ya El Niño. Wanasema kuwa hatua za kukabiliana na majanga zimekuwa zikitilia mkazo utoaji wa chakula na misaada mingine, huku athari za kisaikolojia zikipewa kipaumbele kidogo. Wito huo unakuja wakati serikali kuu na serikali za kaunti zikiongeza kasi ya maandalizi ya kupunguza athari za El Niño katika maeneo yanayokabiliwa na hatari ya mafuriko.
VOX POP-PREPARE