Vijana wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na mpango wa 'Ajira' pamoja na taasisi za Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kupata ujuzi wa kidijitali na wa kiufundi. Wito huo ulitolewa wakati wa hafla ya kuhitimu kwa vijana 330 waliopata mafunzo ya ujuzi muhimu wa kidijitali huko Elgeyo Marakwet. Wito kama huo ulielekezwa pia kwa wanafunzi 267 waliokamilisha kozi ya miezi mitatu na ambao wanatarajiwa kutunukiwa vyeti vya kutambua ujuzi waliokuwa nao awali (Recognition of Prior Learning) katika Kituo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Gichugu.
VOX POP-SKILLS