Kuanzia leo, hakuna shughuli za ujenzi zinazohusisha uchanganyaji wa ballast, saruji na mchanga katika eneo la ujenzi zitakazoruhusiwa kote katika Kaunti ya Mombasa kufuatia agizo la serikali ya kaunti. Gavana Abdulswamad Nassir alisema kusimamishwa huko ni sehemu ya hatua za kupunguza athari zinazotarajiwa za mvua za El Niño. Shughuli za uchimbaji madini na uchimbaji wa visima pia zimesimamishwa kufuatia tathmini ya hali na hatari zinazoweza kutokea kutokana na mvua kubwa inayotarajiwa.
ABDUL NASSIR-SUSPEND