Rais William Ruto amethibitisha tena kujitolea kwa utawala wake kupanua Reli ya Standard Gauge hadi Kisumu akisema mradi huo utanufaisha eneo la Luo Nyanza. Akizungumza mjini Kisumu jana, Ruto alisema Waziri Mkuu wa zamani marehemu Raila Odinga aliunga mkono mradi huo kikamilifu. Alisema kukamilika kwake kutafungua eneo hilo, kuimarisha biashara, kuboresha muunganisho na kurahisisha usafiri wa watu na bidhaa kote Nyanza na eneo lote la Afrika Mashariki.

WILLIAM RUTO –EXTEND