Waziri Mkuu Musalia Mudavadi amekosoa kundi la 'Linda Mwananchi', akisema halijajitayarisha kwa uchaguzi wa mwaka 2027. Mudavadi anasema kuwa licha ya uchaguzi kukaribia, kundi hilo halina chama cha kisiasa wala ajenda iliyo wazi. Aidha, alilikosoa kundi hilo kwa madai ya kutegemea muundo wa chama cha ODM ili kuendeleza ajenda yake ya kisiasa.

MUSALIA MUDAVADI-LINDA