Serikali imeibua wasiwasi kuhusu athari za mila potofu zinazorudisha nyuma elimu ya wasichana katika Kaunti ya Baringo. Waziri wa Jinsia Hanna Cheptumo alisema ndoa za mapema na ukeketaji wa wanawake ni miongoni mwa sababu kuu zinazowalazimisha wasichana kuacha shule mapema. Alitoa wito wa juhudi za pamoja kutoka kwa jamii na wadau kukomesha mila potofu na kuhakikisha wasichana wanabaki shuleni na kukamilisha elimu yao.
HANNA CHEPTUMO-EDUCATION