Kundi la Linda Mwananchi limeahidi kudumisha umoja wake kuelekea uchaguzi wa mwaka 2027. Viongozi wa kundi hilo walikanusha madai ya kuwepo kwa migawanyiko, wakisema watachagua mgombea mmoja wa urais atakayeliwakilisha kundi hilo. Walieleza kuwa mgombea huyo atashauriana na viongozi wengine wa upinzani ili kuunda muungano mpana zaidi na kukubaliana juu ya mgombea mmoja wa kumenyana na Rais William Ruto.
VOX POP-CANDIDATE