Kenya imeimarisha juhudi za kitaifa za ufuatiliaji na mwitikio kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa Mpox katika kaunti arobaini, homa ya Dengue katika kaunti za Garissa na Wajir, pamoja na mkupuko surua katika maeneo kama Baringo na Marsabit. Katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya usalama, serikali imesema kuwa imewasha Mfumo wa Kitaifa wa Kudhibiti Matukio ya Ebola (EVD), licha ya kutokuwepo kwa visa vyovyote vya virusi vya Ebola vilivyogunduliwa nchini. Aidha, mamlaka husika zimetenga maabara maalum na kupeleka timu za mashirika mbalimbali katika vituo vya mipakani ili kuimarisha shughuli za uchunguzi wa afya.