Gavana wa Elgeyo Marakwet, Wisley Rotich, ametoa agizo kwa maelfu ya wakaazi wanaoishi katika maeneo yaliyo na hatari ya kukumbwa na mafuriko na maporomoko ya ardhi kaunti hiyo, ili wahame kabla ya kuwasili kwa mvua inayotarajiwa ya El Niño. Maeneo hayo hatari yapo kando ya miinuko mikali katika Bonde la Kerio, ambapo inakadiriwa kuwa watu elfu 100 wanaishi katika maeneo yaliyo hatarini. Rotich alisema mvua ya El Niño inatarajiwa kuongezeka kufikia mwisho wa mwezi huu, na hivyo ni lazima wakaazi wa maeneo hayo hatari wahame, la sivyo wataondolewa kwa nguvu na serikali.