Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe amezindua mpango wa shilingi bilioni 2.1 wa kujiandaa kukabiliana na athari zinazotarajiwa za El Niño kwa ajili ya mifugo, ili kuwalinda wakulima na wafugaji. Mpango huo unalenga kaunti 24 ambazo hukabiliwa na mafuriko na zina idadi kubwa ya mifugo, huku ukizingatia hatua za mapema ili kuzuia hasara. Waziri Kagwe anasema kuwa El Niño ya mwaka 2023 na mafuriko ya mwaka 2024 yalisababisha hasara kubwa ya mifugo, uharibifu wa miundombinu na mikurupuko ya magonjwa, na serikali inataka wakulima wawe wamejiandaa vyema zaidi wakati huu.