Watoto wawili wenye umri wa miaka mitatu kutoka familia tofauti walizama katika Mto Gathita, katika Kaunti Ndogo ya Tharaka Kusini, Kaunti ya Tharaka Nithi. Watoto hao waliripotiwa kupotea Jumatano, baada ya kushindwa kurejea nyumbani. Wazazi wao walianzisha msako na baadaye wakagundua miili yao isiyo na uhai katika Mto Gathita. Maafisa wa polisi walifika eneo la tukio na kuopoa miili hiyo. Uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa huenda watoto hao walikwenda mtoni kuogelea kabla ya kuzama.