Kiongozi wa DAP-K, Eugene Wamalwa, anatoa wito kwa serikali kuhakikisha mkutano wa Linda Mwananchi uliopangwa kufanyika wikendi hii jijini Nairobi unakuwa wa amani. Wamalwa ameonya dhidi ya kurudiwa kwa vurugu zilizoshuhudiwa Homa Bay, ambapo watu kadhaa waliuawa. Anasema Wakenya wana haki ya kikatiba ya kuunga mkono vyama vya siasa wanavyopenda na hawapaswi kutishwa au kuzuiwa kutekeleza haki hiyo.
EUGENE WAMALWA – RALLY