Serikali imewasihi Wakenya kuwa macho na kutegemea ushauri uliothibitishwa wa serikali huku nchi ikijiandaa kwa mvua inayotarajiwa ya El Niño. Katibu wa Utangazaji Stephen Isaboke anasema hakuna haja ya hofu lakini anaonya kwamba Wakenya wanapaswa kuchukua maandalizi ya mapema kwa uzito na kuendelea kuwa makini na taarifa rasmi. Anawasihi Wakenya kufuata ushauri unaotolewa na serikali na mashirika ya kiufundi, hasa yale mahususi kwa kaunti zao na jamii za wenyeji.
STEPHEN ISABOKE – EL NINO