Mwenyekiti wa Tume ya Jinsia Rehema Jaldesa ameonya kwamba wahusika wa ukeketaji wanabadilisha mbinu, ikiwa ni pamoja na kuifanya tamaduni hiyo hospitalini na kuwapeleka wasichana katika kaunti zingine. Jaldesa anatoa wito wa tahadhari miongoni mwa mashirika ya serikali na umma kutambua na kuripoti visa. Anasema juhudi za pamoja za serikali, mashirika ya kiraia na jamii zinahitajika ili kukabiliana na ukeketaji na kuongezeka kwa visa vya mauaji ya wanawake.
REHEMA JALDESA – TACTICS