Mshukiwa mwenye umri wa miaka 34, anayedaiwa kuwa mwanachama wa genge la uhalifu, amekamatwa eneo la Kondele, Kaunti ya Kisumu, katika operesheni ya mashirika mbalimbali ya usalama iliyopelekea pia kupatikana kwa bangi, silaha butu, mali ya serikali na vifaa maalum vya kiusalama. Mshukiwa huyo, Franklin Okungu – anayefahamika zaidi kwa jina la utani la "Ninjaman" – anadaiwa kuwa mwanachama aliyepata mafunzo katika genge haramu linalojulikana kama "American Marines". Kwa sasa anaandaliwa kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka kadhaa, ikiwemo wizi wa mabavu, kumiliki dawa za kulevya na kujihusisha na uhalifu wa kupangwa.
Advertisement
September 11, 2026
1 min read
Related Topics
Facebook
Loading...
Loading next article...
You've reached the end
Browse all articles
Advertisement
Suggested Articles
Newsletter
Get the latest sports stories delivered straight to your inbox.
Now Playing