Sehemu kadha za Nairobi zitakosa maji kuanzia kesho asubuhi huku Kampuni ya Nairobi Water  ikifunga Kiwanda cha Kusafisha Maji cha Sasumua kwa ajili ya ukarabati wa dharura. Ukarabati huo unatarajiwa kuanza leo na kuendelea hadi kesho asubuhi. Maeneo yaliyoathiriwa ni pamoja na Westlands, Lavington, Kilimani, Upper Hill, Kawangware, Kileleshwa, Uthiru, Kibera, Jamhuri na maeneo ya jirani. Wakaazi wamehimizwa kuhifadhi maji ya kutosha.