Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua amemkosoa Rais William Ruto kuhusiana na ziara yake ya maendeleo katika Kaunti ya Bomet, akishtumu serikali yake kwa kushindwa kutimiza ahadi ilizotoa kwa wakaazi. Gachagua alidai kuwa ziara hiyo ililenga kutuliza hali ya kutoridhika inayoongezeka katika eneo la South Rift, ambapo wakaazi wanahisi kutelekezwa na serikali kuu. Aidha, alidai kuwa Ruto hakuwa na miradi mipya ya serikali kuu ya kuzindua au kukagua, na badala yake anategemea miradi ya kaunti kuonyesha maendeleo.