Waziri wa Mazingira Deborah Barasa anawasihi Wakenya kujiandaa kwa mvua inayotarajiwa ya El Niño, akionya kuhusu mafuriko yanayowezekana katika maeneo yenye hatari kubwa. Waziri Barasa anasema wakaazi wanaoishi katika maeneo yanayokumbwa na mafuriko wanapaswa kuchukua tahadhari za mapema na kufuata ushauri wa usalama kutoka kwa mamlaka. Anasema maandalizi, ikiwa ni pamoja na kujua njia za kuhama na kuhamia maeneo salama inapohitajika, yatakuwa muhimu katika kulinda maisha na kupunguza athari za mvua.

DEBORAH BARASA – SENSITIZATION