Serikali imeanzisha mashauriano yanayolenga kumaliza migogoro inayoathiri Ligi ya SportPesa na kuwezesha kuanza kwa soka ya ushindani. Waziri wa Michezo, Salim Mvurya, jana aliitisha mkutano wa mashauriano na wenyeviti wa vilabu vya Ligi ya KPL katika jengo la Talanta Plaza. Mazungumzo hayo yalitoa fursa ya kusikiliza klabu hizo na kuzingatia mapendekezo ya upatanishi. Mvurya alizihimiza pande zote kuweka kipaumbele kwenye mazungumzo ili kuhakikisha mafanikio ya mashindano ya AFCON 2027 yatakayoandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania.
Kabla ya toleo la 60 la mashindano ya Christie 7s wikendi hii, ambayo itahitimisha msururu wa mashindano ya kitaifa ya raga ya SportPesa Sevens katika uwanja wa RFUEA, kampuni hiyo ya kamari imeahidi kuendeleza ushirikiano wake msimu ujao. Mabingwa KCB watachuana na wenyeji Harlequins, Masinde Muliro na Club Afrique katika Kundi A. Kabras, Blak Blad, NYS na Mean Machine watachuana katika Kundi B, huku Menengai Oilers, Nondies, Leos na Kisumu RFC zikiunda Kundi C. Daystar, Mwamba, Embu RFC na Impala zinakamilisha Kundi D. Huyu hapa ni Willis Ojwang kutoka SportPesa.
WILLIS OJWANG - CHRISTIE 7S
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.