Rais William Ruto leo ataendelea na ziara yake ya siku nne katika eneo la South Rift, huku akiwa na ratiba ya kutembelea kaunti za Kericho na Bomet. Rais anatarajiwa kutembelea eneo la Furaha huko Kipkelion Mashariki na Shule ya Msingi ya Rungut huko Bureti kabla ya kuzindua miradi katika Uwanja wa Kapkatet. Baadaye, atakagua kazi zinazoendelea Kiplokyi na Kapkoros katika eneo la Bomet ya Kati na kutembelea Kamureito huko Sotik.


WILLIAM RUTO - PROMISES