Tume ya Kitaifa ya Jinsia na Usawa imetoa wito wa kuchukuliwa hatua za dharura ili kushughulikia changamoto zinazowakabili waathiriwa wa ukatili wa kijinsia. Tume hiyo imelaumu kuchelewa kwa huduma za serikali na uhaba wa vituo vya hifadhi kwa kuzuia utoaji wa msaada kwa waathiriwa. Mwenyekiti wa NGEC, Rehema Jaldesa, alisema kuwa vituo vya hifadhi vilivyopo havipati ufadhili wa kutosha, jambo linalopunguza uwezo wao wa kutoa huduma bora na zenye ufanisi.

REHEMA JALDESA-INTERVENE