Mke wa Rais, Mama Rachel Ruto, anasema kuwa kutokomeza HIV, mimba za utotoni, pamoja na ukatili wa kijinsia na wa kingono, kunahitaji mkakati wa pamoja unaohusisha serikali, jamii na sekta binafsi. Akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa wadau jijini Nairobi, alihimiza ushirikiano kati ya sekta na taasisi za afya, elimu, huduma kwa watoto, usalama na haki. Mama Rachel alisisitiza kuwa wazazi, walimu, wahudumu wa afya, machifu na viongozi wa dini nao lazima watimize wajibu wao kwa kutambua viashiria vya hatari, kuwasikiliza vijana na kuchukua hatua zinazostahili.
RACHEL RUTO – RESPONSE