Mke wa mama Rais Rachel Ruto ametoa wito wa kuwepo kwa mifumo imara ya ulinzi kwa watoto wanaokabiliwa na unyanyasaji na vurugu. Akizungumza jijini Nairobi, Rachel alisema watoto wanaoripoti unyanyasaji lazima wapate mfumo unaosikiliza, kulinda, kuchunguza na kuchukua hatua. Pia ametoa wito kwa watoto kubaki shuleni, akisema umaskini, mimba za utotoni, hali ya HIV, ulemavu au hali ngumu hazipaswi kukomesha elimu yao kabisa. Aliwasihi wazazi, walimu na viongozi wa jamii kuwa watu wazima salama ambao watoto wanaweza kuwaamini.
RACHEL RUTO – PROTECTION